Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

James Atupwa Jela Miaka 30 kwa Akijaribu Kumbaka Kikongwe

Mahakama ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela James Chingwaru (20), mkazi wa Kijiji cha Mtina, baada ya kupatikana na hatia kwa kosa la kujaribu kumbaka bibi mwenye umri wa miaka 75.

Adhabu hiyo imetolewa Machi 16, mwaka huu na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya hiyo, Ferdinand Philip, chini ya kifungu cha 132 (1), (2)(a) cha Sheria ya Kanuni ya adhabu, Sura ya 16 (R.E. 2022).

Alisema ushahidi uliotolewa mahakamani, mshtakiwa alitenda kosa hilo Disemba 14, 2025 katika kitongoji cha Nyerere, Kijiji cha Mtina wilayani Tunduru, ambako alikamatwa na baadaye kufikishwa mahakamani Januari 13, 2026 kwa hatua za kisheria.

Ilielezwa kuwa mahakama iliridhika kuwa upande wa mashtaka umethibitisha shtaka hilo bila kuacha shaka.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Moshi alisema "Nisisitize umuhimu wa kulinda makundi yaliyo katika mazingira hatarishi, ikiwemo wazee, dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia.".

Aidha, ameeleza kuwa adhabu hiyo inalenga kutoa funzo kwa jamii na kuzuia vitendo vya aina hiyo, huku akiwataka wananchi kushirikiana na vyombo vya dola katika kupambana na uhalifu.

 

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: