Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwigulu Nchemba ameiagiza Sekretarieti ya Maadili kwa Viongozi wa Umma kuanzisha kitengo maalumu kitakachochambua taarifa za mali za Viongozi na kufuatilia kwa ukaribu mwenendo wao wa maadili.
Akizungumza na Sekretarieti hiyo leo Disemba 11, 2025 Amesema hatua hiyo ni muhimu ili kufunga mianya ya rushwa na kuhakikisha Viongozi wanawajibika ipasavyo vilevile amesisitiza kuwa kila Kiongozi anatakiwa kujaza tamko la mali na madeni na Sekretarieti ichunguze kwa kulinganisha taarifa hizo na mapato halisi.
Aidha ameitaka Sekretarieti kushirikiana na Taasisi za uchunguzi katika maeneo yenye viashiria vya rushwa na kuboresha mifumo, kanuni na fomu za maadili ili kuharakisha utekelezaji. “Lazima tuwahofishe wale wasiogopa mali ya umma. Kama mtu hataki kuwa na nidhamu binafsi, basi Serikali italazimisha nidhamu hiyo hakuna yeyote anayepaswa kugusa mali ya umma bila uwajibikaji,” Mwigulu Nchemba.
Chanzo; Millard Ayo