Polisi ya Tanzania imewaonya wote wanaopanga awamu nyingine ya maandamano ya umma ikisema taifa hilo haliko tayari kushuhudia kile imekitaja kuwa "machungu na madhara" yaliyoshuhudiwa wakati na baada ya uchaguzi wa mwezi Oktoba.
Maafisa wa usalama nchini humo wanatuhumiwa kuwaua mamia ya waandamanaji waliojitokeza kupinga uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, ambao ulimrejesha madarakani Rais Samia Suluhu Hassan.
Msemaji wa polisi ya Tanzania, David Misime amesema maandamano mengine yanayopangwa mnamo Disemba 09, 2025 hayakubaliki na yanakiuka haki za raia wengine.
Chanzo; Dw