Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Jaji Chande, Tutaichunguza Oktoba 29 Chanzo na Madhara

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchunguzi wa matukio yaliyotokea siku ya Uchaguzi Mkuu October 29, 2025 na baada ya Uchaguzi, Jaji Mkuu Mstaafu, Mohamed Chande Othman, ametoa wito kwa Watanzania kushirikiana na Tume hiyo ili ipate taarifa sahihi zitakazowesha uchunguzi wenye kuzaa matunda.


Akiongea Jijini Dar es salaam leo December 01,2025, Chande amesema “Tunatoa wito kwa Watanzania, Wadau wote, tushirikiane ili Tuke iweze kupata taarifa sahihi na nasisitiza ya ukweli ambayo itatuwezesha kufanikisha uchunguzi na hadidu za rejea”

Jaji Mkuu Mstaafu Chande ametaja mtiririko wa mambo sita ambayo yatachunguzwa ambayo ni “kuchunguza na kubaini chanzo halisi cha matukio wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi, kuchunguza lengo lililokusudiwa na wale ambao walikuwa wamepanga na kutekeleza vitendo hivyo ili kujua lengo lao”

“Kuchunguza na kubainisha madhara yaliyojitokeza ikiwemo vifo majeruhi uharibifu wa mali na madhara ya kiuchumi na kijamii, kuchunguza mazingira na hatua mbalimbali zilizochukuiliwa na Serikali na vyombo vyake na Mtu yeyote mwingine, kupendekeza maeneo yanayohitaji kuimarishwa zaidi ili kuongeza uwajibikaji wa Viongozi na Raia kwenye kulinda amani ya Tanzania, utawala bora, haki za binadamu, utawala wa sheria hadi kufikia maridhiano ya kitaifa na kuchunguza jambo lolote ambalo Tume itaona ni muhimu na litaendana na majukumu ya Tume”

 

Chanzo; Millard Ayo

Kuhusiana na mada hii: