Watu watano wamekamatwa kwa tuhuma za ulanguzi wa tiketi katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Magufuli jijini Dar es Salaam.
Walikamatwa juzi baada ya kufanyika ukaguzi wa kushtukiza wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini(LATRA), kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.
Baadhi ya walanguzi hao, walikamatwa wakiwa na tiketi za karatasi mkononi ambazo waliwauzia kwa gharama kubwa wasafiri wanaokwenda katika mikoa mbalimbali kupitia kituo hicho cha Magufuli.
Akizungumza baada ya kukamatwa watuhumiwa hao, Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Habibu Suluo, amesema anataka wachukuliwe hatua ili iwe fundisho kwa wengine wanaofanya vitendo kama hivyo.
Chanzo; Nipashe