Mchungani wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) Makimbilio, Manispaa ya Moshi, Jane Mwangalimi amekutwa amefariki dunia nyumbani kwake alikokuwa akiishi na mjukuu wake wa miaka mitano.
Tukio hilo ambalo limetokea Januari 20, 2026 limegunduliwa na mjukuu wake huyo aliyekuwa akiishi naye, Mtaa wa Kariwa Chini, Kata ya Rau, Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro baada ya kumuamsha bibi yake asubuhi kwa muda mrefu bila kuamka.
Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Simon Maigwa amesema baada ya kupata taarifa za tukio hilo walifika eneo la tukio.
Hivyo Polisi wameuchukua mwili wa marehemu na umehifadhiwa hospitali ya KCMC kwa uchaguzi wa Kitabu.
Amesema uchunguzi utafanyika kubaini chanzo cha kifo na taarifa zaidi itatolewa.
Chanzo; Mwananchi