Rais Samia Suluhu Hassan amesema nguvu iliyotumika na Serikali kudhibiti vurugu, iliendana na ukubwa wa tukio lenyewe na kwamba ameapa kuilinda nchi, mipaka yake na usalama wa raia wake.
Ilivyofanywa na Serikali siku hiyo, amesema ndivyo inavyofanyika katika mataifa mbalimbali kunapotokea tukio la vurugu zinazotishia usalama wa raia na Taifa kwa ujumla.
Rais Samia ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam leo, Jumanne Desemba 2, 2025 alipozungumza katika kikao chake na wazee wa jiji hilo.
“Sasa tunapoambiwa kwamba tulitumia nguvu kubwa sana kwenye tukio lile, nguvu ndogo ilikuwa ni ipi? Ilikuwa tuwaangalie waandamanaji waliojiandaa kufanya mapinduzi mpaka wafanikiwe? Hapo patakuwa pana dola kweli, dola haipo hivyo,” amesema.
Rais Samia amesema jambo kama hilo, limeshuhudiwa pia katika maeneo mengine mengi, panapotokea vurugu kama hizo, Serikali hutumia nguvu kubwa kudhibiti.
“Sasa wanapokuja kutulaumu mlitumia nguvu kubwa, wao walitaka nini,?
Chanzo; Nipashe