Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imefanikisha ukamataji wa jumla ya kilogramu 3,799.22 za dawa za kulevya, kuteketeza ekari 18 za mashamba ya bangi pamoja na kutaifisha mali za wahalifu zenye thamani ya shilingi bilioni tatu na milioni mia tatu na nne (3,304,000,000/=) katika operesheni mbalimbali zilizofanyika mwezi Novemba. Jumla ya watuhumiwa 84 walikamatwa kuhusiana na uhalifu huo.
Chanzo; Clouds Media