Wanakijiji wa eneo la Kibaha Muheza, mkoani Pwani, wameiomba Serikali kupitia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kusikiliza na kutatua kero ya ardhi inayowakabili wakazi wapatao 30 katika eneo hilo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wanakijiji hao wamesema wameishi katika eneo hilo kwa zaidi ya miaka 20, wakiwa tayari wamejenga nyumba na kuanzisha makazi yao, lakini sasa wanakabiliwa na madai ya kutakiwa kulipia upya maeneo hayo au kuondoka.
Wamesema hali hiyo imewaletea hofu kubwa, kwani baadhi yao wameishi hapo kwa muda mrefu hadi sasa wana watoto na wajukuu wanaoishi katika eneo hilo.
Wanakijiji hao wameiomba Serikali kuingilia kati mgogoro huo ili kupatikana kwa suluhisho la kudumu litakalowapa haki na kuwalinda na hatari ya kupoteza makazi yao.
Chanzo; Global Publishers