Upepo mkali umeezua na kubomoa nyumba 12 katika vijiji vya Matai B na Kateka wilayani Kalambo, mkoa wa Rukwa.
Maafa hayo yamesababisha watoto saba kujeruhiwa na kuacha familia kadhaa bila makazi baada ya nyumba zao kuharibiwa vibaya na dhoruba hiyo.
Mbali na makazi, wakazi wa vijiji hivyo wameeleza kuwa mvua hiyo imeharibu vibaya mashamba ya mahindi na maharagwe.
Tukio hilo limeacha simanzi kwa wananchi ambao sasa wanakabiliwa na changamoto ya makazi pamoja na hofu ya upungufu wa chakula kufuatia uharibifu wa mazao yao.
Chanzo; Itv