Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amesema kwasasa wanafanyia utafiti camera zinafungwa majumbani kwa watu au sehemu mbalimbali nazo zisajiliwe kama ndege ambazo hazina rubani(drones) kwa sababu baadhi ya camera hizo hutumiwa vibaya na watu kuchunguza maisha ya watu binafsi badala ya dhumuni halisi.
Ameyasema hayo wakati wa mahafali ya Tatu ya Chuo cha Taaluma ya urekebishaji Tanzania kilichopo Magereza Ukonga ambapo amesema wanaendelea kutafakari zaidi na kuchunguza ili watoe muongozo hapo baadae huku akiwataka Chuo hicho kuona haja ya kufunga camera hizo ili kuzuia uhalifu
Aidha amewaagiza Jeshi la Magereza kupita katika magereza kuangalia kama kuna haja ya kuongeza visima kwa ajili ya upatikanaji wa maji ya uhakika mda wote ili kukabiliana na hali inayoendelea sasa ya upumgufu maji yasiwasumbue kabisa.
Kuhusu Ombi la chuo hicho kufungiwa Taa za sola kubwa za barabarani na baadhi ya maeneo mkuu wa mkoa amekubali ombi hilo na kuwataka waandae bajeti na kumpelekea ili waone jinsi ya kulifanyia kazi kwa haraka.
Chanzo; Millard Ayo