Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mzee Mtei Aliukataa Uchawa kwa Vitendo

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amemwelezea mzee Edwin Mtei kama kiongozi wa kisiasa na mtendaji wa Serikali jasiri aliyekuwa na uthubutu wa kuukataa uchawa.

Hotuba hiyo iligusiwa leo kwenye mazishi ya Mtei na Naibu Katibu mkuu wa Chadema (Bara), Aman Golugwa kwamba wamepokea salamu za ujumbe wenye kurasa tisa kutoka gerezani kwa Mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu na itasambazwa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari.

Katika salamu zake hizo alizozipa kichwa cha habari “Hotuba ya Heshima kwa Edwin Mtei” ambazo amezituma kwa waombolezaji akiwa mahabusu kwa zaidi ya siku 280 katika gereza la Ukonga Jijini Dar es Salaam, Lissu alisema maisha yake yalijaa busara tele.

Lissu ambaye anashikiliwa mahabusu kutokana na kesi ya uhaini inayomkabili, alisema ni kutokana na kutofautiana kwake na Rais wa awamu ya kwanza, Mwalimu Nyerere wakati yeye akiwa waziri wa Fedha, aliamua kujiuzulu.

Lissu alisema miaka 94 ya Mtei duniani aliitumia kuwapa Watanzania thamani kubwa na ni maisha yaliyojaa busara na yalikuwa na maana kubwa kwa taifa.

 

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: