Kutoka Ubungo -Chai bora, jijini Dar es Salaam yalipo makao Makuu ya Kanisa la Ufufuo na Uzima lililopo chini ya Askofu Dkt. Josephat Gwajima, Bongo5 imepita na kushuhudia baadhi ya waumini wa Kanisa hilo wakiwa wamejitokeza kwenye viunga vya Kanisa hilo mchana wa leo, Jumanne Novemba 25.2025

Taarifa zinaeleza kuwa waumini hao wamejitokeza kwenye viunga hivyo kufuatia agizo lililotolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba ambaye Novemba 24.2025 alimuagiza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kuhakikisha wanalifungulia Kanisa hilo, ili waumini wake waendelee na ibada huku likiwa kwenye uangalizi maalum, agizo lililoenda sambamba na ‘nyumba’ nyingine za ibada
Chanzo; Bongo 5