Jumla ya wafungwa 1,036 wamepata msamaha uliotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuadhimisha miaka 64 ya Uhuru wa Tanzania Bara Desemba 9, 2025.
Kati yao, 22 wameachiliwa huru leo, huku 1,014 wakipunguziwa adhabu zao na kuendelea kutumikia vifungo vilivyobaki.
Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene kwa niaba ya Rais Samia, ambapo ameeleza kuwa serikali inatarajia wale waliorejea uraiani wataishi kwa kufuata sheria na kushiriki katika ujenzi wa Taifa bila kurudia makosa.
Msamaha huo umetolewa kwa mujibu wa mamlaka ya Rais chini ya Ibara ya 45(1)(a) ya Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977.
Chanzo; Nipashe