Msemaji wa serikali ya Tanzania Gerson Msigwa ameonya vyombo vya Habari vya nje na kutaka vifate maadili ya habari, aidha ametaja vyombo hivyo kama CNN, BBC na DW Ameyasema hayo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.
"Kumejitokeza wimbi kubwa la vyombo vya habari hasa vyombo vya habari vya nje kuchapisha na kutangaza habari ambazo ni za upande mmoja na wakati mwingine kufanya upotoshaji wa taarifa wenye mrengo wa kuchochea chuki kwa watanzania dhidi ya Serikali, kuwagombanisha Watanzania wenyewe kwa wenyewe kutokana na tofauti za kisiasa kidini na kikanda"
"Kuendelea kuyashabikia matukio yale au kuchochea kwa kutangaza na kuchapisha maudhui yenye kuzua taharuki, kupotosha ama kutia hasira watu kwa namna ambayo vyombo vya habari vya nje au wanaojiita wanaharakati au wenye maslahi ya kisiasa wanafanya hakuna manufaa kwa taifa letu"- Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa
Chanzo; Tanzania Journal