Baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) kuwaondolea mashtaka washtakiwa 20 waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka ya uhaini katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu isipokuwa mfanyabiashara Jeniffer Jovin ‘Niffer’ na Mika Chavala, wakili wa utetezi, Peter Kibatala, amefunguka.
Kibatala amesema mteja wake hajahusishwa katika orodha ya walioondolewa mashtaka kutokana na jina lake kukosekana katika majina yaliyotajwa.
Ameeleza kuwa alilazimika kutumia mbinu za kisaikolojia ili kumtuliza na kumjengea uelewa kuhusu hatua hiyo.
Kibatala amesema kuwa, kama wakili wake, ataendelea kutumia nguvu na taratibu zote za kisheria kuhakikisha anamtetea mahakamani.
Aidha, amebainisha kuwa ifikapo Desemba 3 ambayo kesi itatajwa tena, atawasilisha hoja zaidi za kisheria ili kuhakikisha naye pia anapata haki na kuwa huru.
Canzo; Global Publishers