Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, ametoa ruhusa kwa magari ya abiria kuanza kutumia barabara ya Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) Awamu ya Tatu, inayoanzia katikati ya Jiji la Dar es Salaam kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JNIA hadi Gongo la Mboto, kwa lengo la kupunguza msongamano katika barabara ya Nyerere.
Ulega ametoa ruhusa hiyo leo, Novemba 25, 2025, jijini Dar es Salaam, mara baada ya kukagua utekelezaji wa mradi huo, ambao umekamilika kwa asilimia 100. Amesisitiza umuhimu wa barabara hiyo kuendelea kutumika hadi pale mtoa huduma wa kuleta mabasi katika barabara hiyo atakapopatikana.
Ulega amewaeleza wananchi wa Gongo la Mboto kuwa haiwezekani barabara zilizojengwa kwa gharama kubwa zisiweze kutumika, huku watu wakiendelea kukwama kwenye msongamano wa magari kila siku
Chanzo; Global Publishers