Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Benki Kuu Yamwaga Ajira 105 Kada Mbalimbali

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetangaza jumla ya nafasi 105 za ajira katika kada mbalimbali, ikiwakaribisha Watanzania wenye sifa kuomba nafasi hizo kabla ya Machi 24, 2026.

Tangazo hilo lililotolewa Machi 10, 2026 linaeleza kuwa nafasi hizo zinalenga kuongeza nguvu kazi yenye weledi na kuimarisha utendaji wa taasisi hiyo.

 Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, waombaji watakaofanikiwa watapangiwa vituo vya kazi.

Vituo hivyo ni katika ofisi mbalimbali za benki hiyo ikiwemo makao makuu Dodoma, ofisi ndogo za Dar es Salaam na Zanzibar na matawi ya Arusha, Mbeya, Mtwara na Mwanza au katika Chuo cha BoT kilichopo Mwanza.

Nafasi zilizotangazwa zinahusisha kada za kitaalamu, kiutawala na kiufundi. Baadhi ya nafasi hizo ni Ofisa wa Benki Daraja la III (nafasi 16), Mhasibu III (nafasi 11), Bank Examiner III (nafasi 7), Mtaalamu wa Tehama III (nafasi 8) na Computer Analyst/Programmer III (nafasi 6).

Pia zipo nafasi za Mkaguzi wa Ndani (Systems Auditor) III (nafasi 4), Mtaalamu wa Sheria III (nafasi 2), Ofisa Usalama III (nafasi 2), Mtaalamu wa Manunuzi III (nafasi 2), Ofisa Mipango III (nafasi 1), Mtaalamu wa Fedha III (nafasi 1) na Mtaalamu wa Biashara III (nafasi 1).Kwa upande wa kada za uhandisi na ufundi, BoT imetangaza nafasi za Mhandisi Mitambo III (nafasi 1), Mhandisi wa Umeme III (nafasi 1), Fundi Umeme III (nafasi 1) na Electronics Technician III (nafasi 1).

Aidha, zipo nafasi za Muhudumu wa Mapokezi III (nafasi saba), muhudumu wa jikoni III (nafasi tano), Porter III (nafasi mbili), Katibu Muhtasi III (nafasi tatu) pamoja na Walinzi (Security Guard III) nafasi 19.

 

 

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: