Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Wahamiaji Haramu 14 Wakamatwa Mwanza

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linawashikilia wahamiaji haramu 14 raia wa Burundi waliokamatwa wakiwa wameingia nchini kinyume na sheria, kwa kutumia magari mawili tofauti ya abiria.

Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbrod Mutafungwa,leo wilayani Sengerema, wakati akizungumza na umma kupitia vyombo vya habari .

Amesema mafanikio hayo yametokana na ufuatiliaji wa mienendo ya kihalifu pamoja na uwekaji wa vizuizi barabarani .

Anaeleza katika Kijiji cha Busisi, Tarafa ya Sengerema, wahamiaji haramu 13 walikamatwa Novemba 23, 2025 majira ya saa 7:30 mchana wakiwa wanasafiri ndani ya gari aina ya Tata lenye namba za usajili T 337 DYA, mali ya Chiza Francis Lugubi, mkazi wa Dodoma, ambalo husafiri kati ya Kabanga (Ngara, Kagera) na Mwanza.

Wakati wa kukamatwa, dereva wa gari hilo, aliyetambulika kwa jina la Jonas Richard, alitoroka na juhudi za kumtafuta zinaendelea.

Watuhumiwa wengine waliokamatwa kwa tuhuma za kuhusika katika usafirishaji wa wahamiaji hao ni Mustahper Emily (24), fundi magari na mkazi wa Kahama, Shinyanga, pamoja na Pendo Matembere (36), kondakta na mkazi wa Nyegezi, Mwanza.

Baada ya mahojiano, ilibainika kuwa wahamiaji hao waliingia nchini kupitia mpaka wa Kabanga mkoani Kagera mnamo Novemba 22, 2025.

Mtuhumiwa wa 14, Shadia Japhari Majaliwa (18), raia wa Burundi na mkazi wa Kisuru, alikamatwa katika eneo la Nyatukala wilayani Sengerema akiwa ndani ya gari aina ya Yutong lenye usajili T 131 DRE.

Magari yote mawili yanashikiliwa na jeshi la Polisi huku dereva na wasaidizi wengine wakiendelea kuhojiwa kuhusiana na tuhuma za kuwasafirisha wahamiaji haramu.

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: