Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Kifo cha Mwanafunzi Kuchunguzwa, Mtwara

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara limeanza uchunguzi wa tukio la kifo cha Sumaya Hassan Mataka, mwanafunzi wa miaka 12 wa Shule ya Msingi Ufukoni, ambaye mwili wake ulishinda katika fukwe za Bahari ya Hindi, mtaa wa Ufukoni, Wilaya ya Mtwara.

Kulingana na taarifa rasmi ya Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mtwara, marehemu alitoka nyumbani tarehe 21/11/2025 asubuhi na kwenda maeneo ya Magoela akiwa na watoto wenzake, na hakurudi nyumbani. Wazazi na wanakijiji walitoa ripoti kuhusu kutoweka kwake na kuwasilisha taarifa kituoni Mtwara.

Mwili wa marehemu ulibainika tarehe 22/11/2025 majira ya saa 01:30 asubuhi katika fukwe za Bahari ya Hindi, eneo lenye miti ya mikoko, ukiwa na majeraha sehemu mbalimbali na mchanganyiko wa mchanga mdomoni na puani.

Uchunguzi wa awali unaonyesha kifo kilitokana na kukosa hewa baada ya kuwekwa mchanga mdomoni na puani, na kumbukumbu za vitendo vya ukiukwaji wa mwili na unyanyasaji wa kingono, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na polisi.

Polisi wamesema mwili umekabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya taratibu za mazishi, huku uchunguzi wa kina ukiendelea ili kuwakamata wahusika wa tukio hili la kikatili. Jeshi la Polisi Mtwara linatoa wito kwa yeyote aliye na taarifa za tukio hili kuwasiliana na kituo cha polisi Mtwara ili msaada wa kuwakamata watuhumiwa wapatikane kwa haraka.

 

Chanzo; Global Publishers

Kuhusiana na mada hii: