Baadhi ya mabasi ya ‘mwendokasi’ yanayotumia mfumo wa gesi yakiwa katika Kiwanda cha Golden Dragon nchini China.
Mabasi hayo zaidi ya 50 yanayotarajiwa kuwasili nchini mwezi ujao. Mabasi hayo yanayotarajiwa 50 yatatumika katika njia ya mwendokasi awamu ya kwanza ya Kimara- Gerezani- Kivukoni.
Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa, Novemba 28, 2025, Msemaji wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (Udart), Gabriel Katanga amesema mabasi hayo ni kati ya 100 yanatotarajiwa kuwasili nchini na kuanza kutoa huduma ya usafiri.
Katanga amesema, "Basi moja la majaribio liliwasili, yakabaki mabasi 99, sasa haya nayo yakiwa tayari yataanza kuja mabasi 50 kisha yatabaki 49, nayo yatawasili bila shaka haitazidi Desemba au Januari mwakani.’’
Chanzo; Mwananchi