Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Ahukumiwa Kifo, Aliua Mwanae Kisa Utajiri

Mahakama ya Rufaa Kanda ya Iringa, chini ya Jaji Angaza Mwipopo imemhukumu kunyongwa hadi kufa Joseph Yustino Muhulila (28), dereva wa bajaji baada ya kupatikana na hatia ya kumuua kikatili mwanaye wa kiume aitwae Timotheo Joseph, mwenye umri wa miaka minne na miezi sita.

Upande wa Jamhuri uliowakilishwa na Mawakili wawili Mwakalinga na David Mwaibara ambapo Mahakama ilithibitishiwa pasipo shaka kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo la mauaji kwa kukusudia kati ya Aprili 9 na 12, 2025 katika Kata ya Mkwawa, Manispaa ya Iringa, majira ya saa 5:45 usiku.

Ilielezwa Mahakamani kuwa Mshtakiwa, ambaye alikuwa akiishi na mtoto huyo licha ya kutokuwa kwenye ndoa rasmi na Mama wa Mtoto, alimuua kikatili kwa kumkata vipande vidogo vidogo kwa kutumia kisu na kisha kuponda kichwa kwa jiwe. Baada ya hapo, alitupa mabaki ya mwili chooni na kuyaflush ili kuficha ushahidi.

Katika ushahidi uliotolewa Mahakamani hapo ilibainika kuwa awali Mshtakiwa alitoa Taarifa Polisi akidai mtoto amepotea katika mazingira ya kutatanisha, jambo lililoanzisha msako wa kumtafuta mtoto huyo. Hata hivyo, Uchunguzi wa kina uliofanywa na Jeshi la Polisi ulimhusisha moja kwa moja na tukio hilo, na hatimaye alikamatwa na kuhojiwa.

Mbele ya mashahidi wa tano na nane, mshtakiwa alikiri kutenda kitendo hicho, akieleza kuwa alifanya mauaji hayo kwa lengo la kupata utajiri, akidai kuwa alishawishiwa na tamaa hiyo ambapo kwa Upande wa utetezi uliokuwa ukiongozwa na wakili Geofrey Mwakasege uliwasilisha hoja za utetezi, huku Mshtakiwa mwenyewe akitoa ushahidi kwa kiapo akijieleza kuwa ni dereva bajaji na kueleza mazingira ya uhusiano wake na mama wa mtoto. Hata hivyo, Mahakama haikuridhishwa na utetezi huo.

Akisoma hukumu hiyo, Jaji Angaza Mwipopo alisema mahakama imejiridhisha kuwa ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka umejitosheleza kuthibitisha kosa hilo bila kuacha shaka yoyote, hivyo kumkuta mshtakiwa na hatia ya mauaji ya kukusudia, kutokana na hilo, mahakama ilitoa adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa mujibu wa sheria.

 

 

 

Chanzo;  Millard Ayo

Kuhusiana na mada hii: