Mkurugenzi wa Sheria wa CHADEMA, Gaston Garubindi ambaye pia ni Wakili wa Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu amelalamikia utaratibu wa kumuona mteja wake akidai upo kinyume na sheria.
Katika taarifa yake kwa Umma leo, Wakili huyo amedai alipoenda kumtembelea kiongozi huyo kwa masuala yahusuyo kesi yake, alishindwa kuzungumza naye kwa sababu ya kukosekana usiri kati yao.
"Nimeshindwa kutekeleza majukumu yangu kama wakili kutokana na Magereza kulazimisha mazungumzo yangu kama wakili na mteja wangu Tundu Lissu yafanyike mbele ya Maofisa wa Magereza kinyume na Katiba ya nchi, kinyume na sheria ya Magereza, kinyume na kanuni za Kimataifa"
"Hivyo nimekataa kuzungumza na mteja zaidi ili tutafute kwanza haki ya usiri wa mazungumzo kati ya mawakili na mteja wetu." imesema sehemu ya taarifa ya Wakili Garubindi.
Chanzo; Nipashe