Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Moto wa Ajabu Waitesa Familia

Moto wa ajabu ambao huibuka na kuzimwa mara kwa mara umeingia siku ya 13 mfululizo katika mtaa wa Nyantotolotolo “A”, kata ya Nyankumbu, Manispaa ya Geita mkoani Geita, na kuiacha familia moja ikiishi katika hofu kubwa na sintofahamu.

Mama wa familia hiyo, Pendo Sangizyo, amesema moto huo ulianza Januari 6 na hujitokeza ghafla ndani ya vyumba tofauti vya nyumba, ukiteketeza nguo, magodoro na mali nyingine, licha ya kuzimwa kwa kutumia maji kila mara.

Kwa mujibu wa Pendo, hali hiyo imewaathiri watoto wao kielimu, kwani sare za shule zimeteketea na watoto watatu kwa sasa hawahudhurii masomo, huku familia ikilazimika kuishi kwa tahadhari ya kudumu kwa kuandaa ndoo za maji kila asubuhi kusubiri moto unapojitokeza.

Cha kushangaza, moto huo umeendelea kujitokeza hata katika vyumba ambavyo havijaunganishwa na huduma ya umeme, hali iliyofanya chanzo chake kubaki kuwa kitendawili na kuongeza hofu kwa familia hiyo.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Geita limesema limeanza uchunguzi kubaini chanzo cha tukio hilo, huku likitoa wito kwa wananchi kutoa taarifa za mapema pindi matukio ya moto yanapotokea.

 

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: