Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu DSM imewaachia huru watuhumiwa 47 wa kesi ya Uhaini waliokuwa wakishikiliwa tangu Oktoba 29, 2025 kufuatia matukio ya vurugu za baada ya uchaguzi.
Uamuzi wa kufuta mashtaka hayo umetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Ushindi Swalo . hatua hiyo imechukuliwa baada ya upande wa Mashtaka kupitia Wakili wa Serikali Mkuu Job Mrema kuwasilisha ombi la Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) la kutokuwa na nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya watuhumiwa hao 47 kati ya 48 waliokuwa wanakabiliwa na tuhuma hizo.
Mshtakiwa mmoja kati ya 48 ambaye Naslin Lawrence Mkangala maarufu Luponzi yeye hajaachiwa na amerudishwa Mahabusu.
Chanzo; Millard Ayo