Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mo Dewji, Bilioni 25 kwa Vijana Wabunifu wa AI

Bilionea Mohammed Dewji, ambaye pia ni Mwenyekiti Mtendaji wa MeTL Group, kuanzisha mfuko wa ubunifu wenye lengo la kukuza sekta ya teknolojia nchini Tanzania na barani Afrika.

Mfuko huu wenye thamani ya shilingi bilioni 25, unalenga kutoa msaada kwa vijana wenye mawazo ya kisasa, hasa katika maeneo ya teknolojia, akili bandia (AI), fintech, na ujasiriamali wa kiteknolojia.

“Niko mbioni kuzindua Mfuko wa Ubunifu (Startup Fund) wenye thamani ya shilingi bilioni 25 kusaidia wana teknolojia, akili bandia (Al), fintech, na wabunifu wa kiteknolojia hapa Tanzania na Afrika. Tutatoa michango na uwekezaji kusaidia vijana wabunifu wenye mawazo ya kubadilisha dunia.
Andaieni mawazo yenu muda umefika.”

Mfuko utatoa ruzuku, uwekezaji, na msaada wa aina mbalimbali ili kuwasaidia wabunifu katika hatua za mwanzo za miradi yao.

Lengo kuu ni kukuza uchumi wa kidijitali na kutoa fursa kwa vijana kuchangia kwenye mageuzi ya teknolojia ambayo yanaweza kuleta athari kubwa katika jamii na uchumi wa taifa.

Dewji ni mmoja wa wafanyabiashara maarufu barani Afrika, na ameonesha ni jinsi gani ana uwezo wa kuhamasisha na kuchochea maendeleo katika sekta ya biashara na teknolojia.

Anasema kuwa lengo lake ni kuhakikisha kuwa Tanzania na Afrika kwa ujumla zinapata nafasi ya kuongoza katika uvumbuzi wa teknolojia ya kisasa.
 
 
 
Chanzo; Bongo 5

Kuhusiana na mada hii: