Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Chungu za Oktoba 29 Mbeya

Athari ya vurugu na maandamano yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu yameanza kung’ata kufuatia wananchi na viongozi jijini Mbeya kulalamikia mazingira yasiyo rafiki katika kutoa na kupata huduma kufuatia matukio ya uchomaji moto ofisi za serikali za mitaa na kata.

Oktoba 29 zilizuka vurugu na maandamano katika baadhi ya maeneo nchini, ambapo kwa Mkoa wa Mbeya zipo sehemu zilizoathirika ikiwamo miundombinu ya barabara, mali binafsi na ofisi za serikali kuchomwa moto.

Kwa upande wa Jiji la Mbeya, jumla ya Ofisi za kata 13 na ofisi za mitaa 28 zilivamiwa na kuchomwa moto na sasa baadhi ya wananchi na viongozi wa serikali wameanza kupata changamoto kwenye kutoa na kupata huduma.

Mwananchi imefika eneo hilo na kujionea shughuli zinavyofanyika, huku baadhi ya viongozi wa mtaa wakitolea huduma nje kutokana na kutokuwa na vitendea kazi kufuatia nyaraka na samani zote kuungulia ndani.

Kutokana na changamoto hiyo, viongozi wa serikali ya mtaa wa Mapelele na wale wa ofisi ya kata wamehamia jengo la Polisi Kata, huku wakitumia vyumba viwili tu kutoa huduma, hali inayowapa wakati mgumu wananchi na watendaji wenyewe.

Mmoja wa viongozi ambaye hakutaka jina lake kutajwa, amesema wanapitia magumu muda mwingine kutoa huduma nje kwa kuwa hawana kitendea kazi chochote na wakati mwingine hutumia ofisi moja na wataalamu.

 

 

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: