Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Niffer Kuendelea Kusota Gerezani Kesi ya Uhaini

Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP) amewafutia mashtaka na kuwaachia huru washtakiwa 20 kati ya 22 waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya uhaini.

Hata hivyo, Mfanyabiashara wa vipodozi Jenifer Jovin (26) maarufu Niffer, ambaye ni mshtakiwa wa kwanza katika ya uchunguzi wa awali (PI) namba 26388 ya mwaka 2025 na mshtakiwa wa 17 katika kesi hiyo Mika Lucas Chavala, wataendelea kubaki rumande kutoka na DPP kutokuwafutia mashtaka yao.

DPP amewafutia kesi hiyo ya uchunguzi namba 26388/ 2025 chini ya kifungu namba 92(1) cha Sheria ya Makosa ya Jinai, Sura ya 20 ilivyofanya marejeo mwaka 2023.

Uamuzi wa kuwafutia kesi hiyo kwa washtakiwa 20, umetolewa leo Jumanne, Novemba 25, 2025 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Aaron Lyamuya, baada ya Wakili wa Ssrikali, Titus Aron kuieleza Mahakaka hiyo kuwa DPP hana nia ya iuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa 20 kati ya washtakiwa 22 wanakabiliwa na kesi hiyo.

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: