Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limethibitisha kwamba mtawa aitwaye Silianus Balyalemwa Korongo aliyetoweka kutoka kwenye nyumba ya malezi ya Watawa iliyopo katika Kata ya Tungi Mkoani Morogoro, amepatikana katika Jiji la Lusaka, nchini Zambia akiwa salama.
Taarifa ya jana Desemba 4, 2025 iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama imeeleza kuwa Mtawa huyo amepatikana akiwa katika nyumba ya malezi ya watawa iitwayo St. Boniventure University.
Aidha taarifa hiyo imebainisha kuwa kupatikana kwake kumethibitishwa na mtawa mlezi wa nyumba hiyo aitwae Alfigio Tunha, mtawa na mkazi wa Zambia huku Jeshi hilo likiwashukuru wote walioguswa na kusaidia taarifa za kuwezesha kupatikana kwake.
Chanzo; Itv