Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Viongizi Tamesa Kufikishwa Mahakamani Ubadhilifu wa Fedha, Wasimamishwa Kazi

Serikali imemsimamisha kazi Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kupisha uchunguzi wa tuhuma za uzembe, usimamizi dhaifu na ubadhirifu unaowahusu baadhi ya viongozi wa taasisi hiyo.

Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, ametangaza uamuzi huo leo jijini Dar es Salaam baada ya kufanyika kwa uchunguzi ulioanzishwa kufuatia malalamiko ya wananchi pamoja na barua iliyoandikwa kwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ikieleza kuharibika kwa utendaji wa Temesa.

Uchunguzi huo ulibaini ubadhirifu wa takribani Sh bilioni 2.5, hatua iliyosababisha kuundwa kwa kamati maalum yenye siku saba kuchunguza kwa kina. Ulega amesema yeyote atakayebainika kuhusika atafikishwa kwenye vyombo vya sheria bila kusita.

Amesema viongozi wa Temesa wamesimamishwa kazi kwa kushindwa kwenda sambamba na kasi ya maendeleo ya serikali, na uchunguzi wa ndani utaendelea ili hatua za kinidhamu zichukuliwe.

Katika hatua nyingine, Waziri Ulega akiwa katika ziara ya kukagua ujenzi wa kivuko cha Nyinyi–Nyamisati, amesema mradi huo uko nyuma ya muda kwa kuwa umefikia asilimia 57 tu, kinyume na ratiba ya awali ya kukamilika Desemba 2025. Taarifa mpya zimeonesha kuwa mradi huo huenda ukakamilika Mei 2026.

Kivuko hicho kitakuwa na uwezo wa kubeba abiria 300, mizigo tani 120 pamoja na sehemu ya kuhifadhi maiti.

Waziri pia ametembelea ujenzi wa daraja la Nguva Kigamboni na kuagiza liwe limekamilika kufikia Januari 2026. Aidha, amewataka mafundi kurekodi na kushiriki video za kazi zao mtandaoni ili kuwahamasisha vijana kuona manufaa ya miradi ya serikali.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Temesa, Moses Rajabu, amesema mradi wa kivuko hicho unagharimu Sh bilioni 9.4, ambapo Sh bilioni 4.3 tayari zimelipwa.

Mbunge wa Kigamboni, Sanga Nyakisa, ameomba wizara kuharakisha maboresho ya vivuko katika eneo hilo, akisisitiza uhitaji wa ufumbuzi wa kudumu kwa foleni sugu katika vivuko vya MV Kigamboni, Kivukoni na MV Kazi.

 

Chanzo; Global Publishers

Kuhusiana na mada hii: