Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Kijana Atuhumiwa Kumbaka Bibi Yake

Obadia Mpenzu (22), mkazi wa Kitongoji cha Majimoto, Kijiji cha Nanyala, Wilaya ya Mbozi, anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumbaka na kumjeruhi bibi yake mwenye umri wa miaka 80, Tabia Sengo.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Nanyala, Maneno Mwambunga, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo limetokea usiku wa Desemba 8, 2025. Ameeleza kuwa mtuhumiwa alitekeleza kitendo hicho cha ukatili baada ya kufika nyumbani kwa bibi yake majira ya saa nne usiku, wakati mume wa bibi huyo alikuwa kilabuni.

Baada ya tukio hilo, mtuhumiwa alikimbilia sehemu isiyojulikana, na uongozi wa kijiji ulianzisha msako ulioendelea hadi asubuhi ya Desemba 9. Majira ya saa tano asubuhi, mtuhumiwa alikamatwa akiwa amejificha porini, akiwa na dalili za kudhaifu kiafya, akitapika na kudaiwa alikuwa amekunywa sumu kwa lengo la kujitoa uhai kutokana na majuto.

Mtuhumiwa alihamishiwa katika Kituo cha Afya Nanyala kwa matibabu ya dharura kabla ya kukabidhiwa polisi kwa hatua zaidi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Augostino Senga, amesema hali yake ya afya inaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu. Uchunguzi wa tukio hilo unaendelea, na mara ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: