Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Kichanga Chatelekezwa Nyumba ya Wageni Nzega

Mwanamke mmoja asiyejulikana ametelekeza kichanga cha siku tatu katika nyumba ya wageni wilayani Nzega, mkoani Tabora, na kutoweka kusikojulikana.

Tukio hilo limemlazimu Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Bi. Naitapwaki Tukai, kutoa wito kwa mzazi huyo ajisalimishe huku akiahidi zawadi ya shilingi laki tano kwa yeyote atakayesaidia kumpata ili mtoto apate haki ya kunyonyeshwa na kulelewa na mama yake.

Mkuu huyo wa wilaya amesisitiza kuwa hana nia ya kumchukulia hatua za kisheria mama huyo, bali amedhamiria kushirikiana naye katika malezi ya mtoto endapo atabainika kuwa na hali duni ya kimaisha.

Amewasihi wananchi kutoa ushirikiano ili kuokoa maisha ya kichanga hicho ambacho kwa sasa kinahitaji upendo na uangalizi wa karibu wa mzazi wake.

 

 

 

Chanzo; Itv

Kuhusiana na mada hii: