Waziri Mkuu wa Tanzania, Dk Mwigulu Nchemba, leo Jumatatu, Novemba 24, 2025 anafanya ziara ya ukaguzi vituo vya mwendokasi akianzia eneo la Kimara, Barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam.
Katika ziara hiyo, Dk Mwigulu ameongozana na Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, George Simbachawene, Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila.
Ukaguzi huo wa vituo vya mwendokasi unafanyika kufuatia maandamano ya Oktoba 29, 2025 ambayo yalisababisha vurugu zilioharibu miundombinu ya usafiri huo ikiwamo mabasi katika sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam.
Chanzo; Mwananchi