Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro amemesema kuwa majukumu ya Jeshi la Polisi ni kuhakikisha Wananchi wanaishi bila hofu na katika kufanikisha hilo wanahakikisha wanashirikiana na Wananchi wenyewe ili kutokomeza vitendo vya uhalifu na kuhakikisha amani inakuwepo.
Muliro ameyasema hii leo December 05, 2025 wakati akizungumza katika Mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila na Wahariri wa Vyombo vya Habari ambapo amesisitiza “Polisi jukumu lake kubwa ni kuhakikisha Watu wanaishi kwenye mazingira yasiyo na hofu na Watu walindwe”
“Nikubaliane na lile ambalo Wahariri mmetukumbusha la kuhakikisha mnakuwa salama ili mzipate taarifa vizuri na tunaamini mngezipata vizuri taarifa tungeepuka taharuki zilizojitokeza kwahiyo tukiri hilo tutalitekeleza ili mzunguke mueleze hali halisi ya mambo na wala hatutaki mtupendelee”
“Sisi tutaendelea kusimamia sheria kuona Dar es salaam inakuwa salama na Wahariri na Wananchi wengine kwa ujumla mtekeleze majukumu yenu bila hofu” - Muliro.
Chanzo; Millard Ayo