Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mbowe na Maumivu ya Taifa Msibani

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo aliyepita Freeman Mbowe, mbele ya Waziri Mkuu Dr. Mwigulu Nchemba katika mazishi ya Mmoja wa Waasisi wa CHADEMA Tengeru Arusha, amesema bado Taifa la Tanzania lina maumivu hivyo ameitaka Serikali kuhakikisha inarejesha haki na uhuru wa Watu katika Nchi yao.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu na Viongozi wenzako wa Serikali Taifa letu bado lina maumivu makubwa sana na nitakuwa Mnafiki au Mswahili nisipolisema hili, maendeleo ambayo umetueleza kwamba Serikali itasimamia ni jambo jema tunashukuru lakini hakuna jambo la maana na la muhimu kuliko uhuru wa Watu katika Nchi yao” - Mbowe.

“Hawa Viongozi wangu wa Chama chetu wana maumivu, Magerezani wamejaa Viongozi ambao wanastahili kuungana na Watanzania wenzao kuyaona matunda ya Nchi yao, njia bora kuliko zote za kuleta maendeleo katika Nchi yetu rejesheni kwanza uhuru wa Watu, furaha ya Watu, haki za Watu na muukiri ukweli pale ambapo Serikali imekosea isione aibu kusema tulikosea hapa, nina uhakika hata Viongozi wa Chama changu watakuwa tayari kuwasikiliza ili tuitafute kesho iliyo bora katika Nchi yetu” - Freeman Mbowe. 

 

 

Chanzo; Millard Ayo

Kuhusiana na mada hii: