Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Butiku Asema Mazungumzo Yatatatua Migogoro Yetu

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation, Mzee Joseph Butiku, ametaja masuala muhimu yatakayojadiliwa katika Mkutano wa Wazee unaofanyika leo, Januari 22, 2026, yakihusisha ujenzi wa amani, utatuzi wa migogoro na maridhiano ya kitaifa.

Akizungumza katika mkutano huo Butiku alisema kuwa ujenzi wa amani ndio msingi wa majadiliano hayo “Ujenzi wa amani ndio tulianza nao, ukifuatiwa na utatuzi wa migogoro na maridhiano. Tumekuja hapa kutoa ushauri kwa sababu sisi ni Wazee. Baba wa Taifa alitufundisha kuwa mgogoro wowote iwe ni kati ya Watu au Mataifa unaweza kutatuliwa kwa mazungumzo,” alisema Butiku.

Aliongeza kuwa mkutano huo unalenga kuwahimiza Wazee kuongoza Jamii katika kujadili changamoto zao kwa busara, huku akisisitiza kuwa Watanzania bado wana uwezo wa kujitambua na kuzungumza kwa hekima, pamoja na Vijana ambao bado wana nguvu na dhamira ya kushiriki katika kujenga amani ya Taifa.

 

 

 

Chanzo; Millard Ayo

Kuhusiana na mada hii: