Jeshi la Polisi nchini Tanzania limetoa onyo kali kwa makundi na watu binafsi wanaotoa kauli za uchochezi, likisisitiza kuwa litaendelea kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wale watakaobainika kuvunja sheria.
Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi hilo la polisi, kauli za uchochezi zinaweza kuhatarisha amani na utulivu wa taifa, hivyo hazitavumiliwa kwa namna yoyote.
Hivi karibuni kumekuwepo na mfululizo wa matamko kutoka makundi mbalimbali na hata watu binafsi kuhusiana na vurugu zilizotokea wakati na baada ya uchaguzi wa Oktoba 29, hali ambayo imeibua mjadala mpana kuhusu usalama na mustakabali wa amani nchini humo.
Chanzo; Dw