Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mohamed Mtanda, ametolea ufafanuzi video clip inayotaja kutokea Mwanza inayoonyesha wananchi wameandamana na wanasikilizwa na Wanajeshi.
Mtanda akizungumza na vyombo vya habari amewashukuru Wananchi wa Mwanza kwa kuendelea na utulivu na kuitolea ufaanuzi video clip hiyo inayosambazwa ikionyesha kuwa Mwanza wananchi wameandamana na wanasikilizwa na wanajeshi.
RC Mtanda amesema 'Clip hiyo ya zamani ilirekodiwa tarehe 31 Oktoba baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29, kwa hivi sasa vyombo vya usalama vimenihakikishia na mimi mwenyewe nimejiridhisha, nimepita maeneo na mitaa mbalimbali nikiangalia baadhi ya wananchi wakiendelea na shughuli zao, hakuna mkusanyiko wowote unaoendelea' RC Mtanda.
Chanzo; Clouds Media