Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Chadema Wakamatwa Mbeya

Viongozi wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Mbeya wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa madai ya kufanya kusanyiko bila kibali.

Tukio hilo limeelezwa kutokea leo Jumatano, Januari 21 katika Kata ya Inyala Wilaya ya Mbeya wakati viongozi hao walipokuwa kwenye maadhimisho ya miaka 33 ya kuasisiwa kwake.

Waliokamatwa ni Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa, Masaga Kaloli na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (Bavicha), Elisha Chonya.

Akizungumza na Mwananchi, Katibu wa chama hicho, Hamad Mbeyale amesema leo walikuwa programu ya maadhimisho ya miaka 33 ambayo walipanga kufanyia Inyala wilayani humo.

Amesema katika maadhimisho hayo, ilikuwa imepangwa ratiba na matukio tofauti ikiwamo bonanza la michezo, kupata chakula cha pamoja wanachama na kushusha bendera nusu mlingoti kuenzi kifo cha mwasisi, Edwin Mtei aliyefariki dunia Januari 19, 2026, nyumbani kwake Tengeru, mkoani Arusha.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga viongozi hao walikamatwa kwa tuhuma za kuhamasisha watu kufanya mkusanyiko isivyo halali.

 

 

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: