Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Samia Asema Vurugu Zilipanga Kuangusha Dola, Tutailinda Tulivyoapa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amesema vurugu zilizotokea zilikuwa maalum na zilipanga kuiangusha dola ya Watanzania.

Akizungumza na Baraza la Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa niaba za Watanzania, Rais Samia amesema waratibu walidhamiria kuangusha dola la Tanzania kama ilivyotokea nchini Madagascar.

Akifafanua amesema, Serikali imeapa kuilinda amani na mipaka ya nchi ya Tanzania kwa namna yoyote ile, lakini baadhi ya watu wanadai tumetumia nguvu kubwa kudhibiti waandamanaji na kusababisha vifo.



" Wanadai nguvu iliyotumika haikuendana na vurugu, waandaaji wanataka waandamanaji waachiwe wajikusanye waende kuiangusha dola?, tumeona nchi zingine watu kama hao wakiachiwa wanasababisha madhara zaidi, sisi tutailinda dola kama tulivyoapa kwa gharama zozote zile," alisema Rais Samia.

 

Chanzo; Clouds Media

Kuhusiana na mada hii: