Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Ngorongoro Yazidi Kugeuka Dhahabu Duniani

Rais Samia Suluhu Hassan amesema maeneo ya Hifadhi ya Ngorongoro, Pori la Akiba Poleleti na Ziwa Natron ni muhimu sana kwa Taifa, si tu kwa urithi wa ikolojia bali pia kwa rasilimali madini yanayotafutwa duniani.

“Nimesikiliza kwa kina taarifa za tume zote mbili na kutazama makala ya video iliyoonyesha hali halisi ya maeneo mliyoyatembelea.

Mbali ya mambo yaliyonyeshwa hapa na yaliyozunguzwa kuna vitu sasa tunaanza kujua viko kwenye maeneo yale ni muhimu kwa Taifa letu, kuna madini yanayotafutwa duniani yapo kwenye maeneo yale, yapo kwenye Taifa letu,” amesema Samia.

Rais Samaia ameyasema hayo leo Alhamisi, Machi 12, 2026, Ikulu Chamwino jijini Dodoma, wakati akipokea ripoti mbili za tume alizoziunda, kuchunguza kuhusu eneo hilo la Ngorongoro.

 

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: