Mwasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edwin Mtei, na aliyekuwa Gavana wa kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), amefariki dunia.
Mzee Mtei (94) ambaye alikuwa Gavana wa BoT kuanzia 1966 na miaka 12 baadaye akaja kuwa Waziri wa Fedha na Mipango amefariki usiku wa kuamkia leo Januari 20, 2026.
Ameitumikia nafasi ya Waziri wa Fedha na Mipango kuanzia 1978 mpka 1981 alipojiuzulu wadhifa huo.
Akizungumza na Mwananchi asubuhi hii, Freeman Mbowe ambaye amewahi kuwa Mwenyekiti wa Chadema amesema, Mzee Mtei ameugua kwa kipindi kirefu na hali yake ilibadilika ghafla na wakati wanamchukua kwa gari la wagonjwa kumpeleka hospitali ya Seliani na kufariki dunia akiwa njiani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, John Heche, imeeleza kuwa chama hicho kimepoteza moja ya nguzo imara sana.
Chanzo; Mwananchi