Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kimekutana na zaidi ya walimu viongozi 400 kutoka mikoa sita ya Nyanda za Kusini na Mashariki, kujadili changamoto na masuala mbalimbali ya kiutumishi ambapo katika mkutano huo, viongozi wa chama wameiomba Serikali kuwapunguzia walimu mzigo wa kusimamia miradi ya ujenzi wa shule, ili kuwapa nafasi zaidi ya kujikita katika ufundishaji na kuongeza ufaulu wa wanafunzi.
Rai hiyo imetolewa na Rais wa CWT, Dkt. Sulemani Ikomba, wakati wa mkutano wa walimu wa Kanda ya Kusini na Mashariki (SETCO) uliofanyika katika Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma.
Chanzo; Itv