Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

CUF Pamoto Mwenyekiti Ajiuzulu

Wakati Mwenyekiti mpya wa Chama cha Wananchi (CUF), Mirambo Yusuf akianza juhudi za kufanya maridhiano ya ndani, upande unaompinga umedai mchakato huo hautakuwa na maana iwapo hatajiuzulu.

Mirambo, aliyechaguliwa Februari 22, 2026 kuongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka mitano ijayo, yupo katika ziara ya kujitambulisha kwa viongozi wa chama ngazi ya wilaya na wanachama, sambamba na juhudi za maridhiano.

Uchaguzi uliomweka madarakani ulizua mjadala baada ya kufanyika kufuatia maelekezo ya Msajili wa Vyama vya Siasa ya kutengua uchaguzi uliomweka madarakani mtangulizi wake, Ibrahim Lipumba pamoja na viongozi wenzake, uliokuwa umefanyika Desemba 18 na 19, 2024.

Msajili alifuta matokeo hayo akieleza washindi hawakupata zaidi ya nusu ya kura za wajumbe waliopiga kura, hivyo uchaguzi ulipaswa kurudiwa kwa mujibu wa Katiba ya chama ya mwaka 1992 na kanuni zake.

Uamuzi huo ulisababisha mgawanyiko ndani ya chama, ambapo baadhi ya wanachama waliunga mkono hatua ya Msajili huku wengine wakipinga na kuamua kwenda mahakamani.

Mirambo amesema yuko tayari kuzungumza na wanaopinga ushindi wake, iwe kupitia mahakama au kwa Msajili wa Vyama vya Siasa.

“Tutawawekea utaratibu ili tufanye maridhiano. Lazima tuweke msingi mzuri wa kumaliza tofauti zetu,” amesema.

 

 

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: