Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Maafisa Watatu Uhamiaji Wahukumiwa Kunyongwa Hadi Kufa

Mahakama Kuu ya Tanzania imewahukumu kunyongwa hadi kufa maafisa watatu wa Uhamiaji, Fredrick Kyomo, Joachim Trathizius na Mabruki Hatibu, baada ya kupatikana na hatia ya kumuua Enos Elias, mkazi wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma, aliyekuwa akishukiwa kuwa si raia wa Tanzania.

Hukumu hiyo imetolewa Desemba 15, 2025, na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Augustine Rwizile, ambaye alisema ushahidi uliowasilishwa mahakamani umebainisha wazi, bila kuacha shaka yoyote, kuwa mauaji hayo yalitekelezwa na maafisa hao watatu pekee.

Katika hukumu yake, Jaji Rwizile alieleza kuwa upande wa mashtaka uliwasilisha ushahidi wa kutosha uliothibitisha kuwa watuhumiwa walihusika moja kwa moja katika tukio la mauaji, na kwamba hakuna mtu mwingine au kundi jingine lililohusika katika kifo cha marehemu.

Mahakama ilisisitiza kuwa vitendo vilivyofanywa na maafisa hao ni kinyume cha sheria, maadili ya utumishi wa umma na haki za binadamu, na kwamba hukumu hiyo ni funzo kwa watumishi wa umma kuzingatia sheria na taratibu wanapotekeleza majukumu yao.

Kwa uamuzi huo, Mahakama Kuu imewaamuru watuhumiwa hao wanyongwe hadi kufa kwa mujibu wa sheria za nchi.

 

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: