Watoto wawili wa familia moja katika eneo la Katanini Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro wamefariki dunia kwa kutetekea kwa moto, chanzo cha moto huo hakijajulikana.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani hapa, Jeremiah Mkomagi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo leo Desemba 17,2025 saa 5 asubuhi na kuwataja waliofariki kuwa ni Geriel Shayo(4) na Leon Shayo(2).
Chazo; Mwananchi