Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete amesema kuwa katika Jamii kumekuwa na malalamiko makubwa juu ya maadili ya Viongozi wa Umma na ameagiza kuwa Viongozi wote wanaolalamikiwa na Wananchi waitwe wahojiwe ikiwemo yeye mwenyewe juu ya tuhuma zinazowakabili.
Ridhiwani ameyasema hayo wakati akizungumza na Watumishi wa Wizara ya Utumishi wa Umma ambapo amesisitiza kuwa ni vyema taarifa za Watumishi wa Umma zikawa wazi na Viongozi wenye tuhuma wahojiwe na amesema hata yeye aitwe ahojiwe juu ya tuhuma za umiliki wa kituo cha mafuta cha Lake ili ukweli ujulikane na wenye uthibitisho wajitokeze wauseme na ukweli utakapo julikana uwekwe hadharani ili kuweza kuisadia Serikali.
“Nyie wenyewe mnaona maandamano kwa mafano yaliyotokea juzi hapa malalamiko makubwa yalikuwa juu ya maadili ya Viongozi wa Serikali, Tunalalamikiwa Viongozi, kuna mtu mmoja anaitwa Ally Edha ana Vituo vyake vya mafuta vya Lake zadi ya 92 vimechomwa vile kwa sababu vinasemwa ni vya Ridhiwani kaniambia sasa fikiria mtu vituo vyake vya mafuta vinachomwa kwa sababu tu wanahisi fulani ndio anamiliki, sasa nyinyi tuiteni anzeni na mimi Waziri wenu” - Ridhiwani Kikwete
Chanzo; Millard Ayo