Hadija Jumaa, mama wa watoto wanne mkazi wa mtaa wa Mji Mpya mjini Handeni, ameuawa usiku wa kuamkia juzi baada ya kutokea ugomvi na mwanaume aliyekuwa akiishi naye. Tukio hilo limetokea katika Kata ya Mdoe, ambapo inadaiwa mgogoro baina ya wawili hao ulipelekea mauti ya mama huyo.
Balozi wa mtaa huo, Bakari Abdala Kidebwe, pamoja na ndugu na majirani wa karibu na kituo cha mabasi cha Chogo, wamethibitisha kutokea kwa mauaji hayo yaliyoacha simanzi kubwa. Kwa sasa, taarifa zaidi zinaendelea kukusanywa huku jamii ikilaani kitendo hicho kilichofanywa na mtu aliyekuwa akiishi naye kama mume na mke.
Chanzo; Itv