Mary Timotheo, Mkazi wa Garijembe anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wake aitwaye Scola Athanas Mwaba (10) aliyekuwa Mwanafunzi wa Darasa la Nne katika Shule ya Msingi Ngonde.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya SACP Benjamin Kuzaga, amesema tukio hilo limetokea Desemba 09, 2025 saa 6:30 mchana katika Kijiji cha Garijembe, Kata ya Tembela, Wilaya ya Mbeya baada ya Mary Timotheo (mama mzazi wa marehemu) kumuadhibu kwa kumpiga na kitu kizito kichwani, kwa madai ya utukutu.
Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo, ni kujichukulia sheria mkononi kwa kumuadhibu mtoto wake kwa kumpiga hadi kufa na kisha kuutupa mwili wake shamba la jirani na nyumba yake, kwa kushirikiana na jirani yake aitwaye Sharifa Nzalanje, Mkazi wa Garijembe ambaye pia anashikiliwa na Jeshi la Polisi.
cHANZO; Itv