Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mwambe Tuhuma ya Njama ya Kumuua IGP na Uchochezi

Mwambe aachiwa kwa dhamana, atuhumiwa kutaka kumuua Mkuu wa Polisi

Aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na baadae Viwanda na Biashara, Geofrey Mwambe ameachiwa kwa dhamana katika Kituo cha Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa wakili wa Mwambe, Hekima Mwasipu amesema mteja wake aliachiwa kwa dhamana jana Desemba 14, 2025 na kwamba dhamana hiyo imetolewa na Jeshi la Polisi lenyewe.

Mwasipu amesema kuwa myteja wake huyo anatuhimiwa kwa makosa mawili ya jinai ikiwemo kumtishia kumuua Kamanda Mkuu wa Polisi ambaye hata hivyo hajatajwa jina lake, pamoja na tuhuma za kiuchochezi za kimtandao.

Amesema maombi hayo ambayo yalitarajiwa kufanyika leo Jumatatu Desemba 15 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu hayana nguvu tena kwa sababu mteja wake yupo huru.

Kwa upande mwingine Wakili Mwasipu amesema Mwambe ataendelea kuripoti katika ofisi ya ZCO katika kipindi hiki ambacho upelelezi unaendelea na kama atabainika kuwa na kosa, basi atafikishwa Mahakamani.

Itakumbukwa kuwa kwa mujibu wa taarifa ya Polisi ilieleza kuwa Mwambe alikamatawa Desemba 7, 2025 katika eneo la Tegeta, Kinondoni.

 

 

Chanzo; Bongo 5

Kuhusiana na mada hii: